Tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliye juu kwa kutuwezesha kukamilisha kikamilifu huduma ya kuwahudumia wajane katika eneo la Lugeye. Upendo na ushirikiano wenu umerudisha tabasamu na matumaini makubwa kwa mama zetu hawa.
Katika huduma hii iliyofanyika, tumeweza kufanikisha yafuatayo:
- Msaada wa Kifedha: Jumla ya Tsh 429,000/= imegawanywa na kukabidhiwa moja kwa moja kwa wajane ili kuwasaidia katika mahitaji yao ya msingi.
- Msaada wa Mavazi: Tumewapatia wajane nguo na viatu vya kuwasitiri.
- Mawasiliano na Intaneti: Tsh 70,000/= kwa ajili ya huduma ya WiFi na Tsh 20,000/= kwa ajili ya salio/huduma za simu ili kurahisisha mawasiliano wakati wa zoezi hili.
- Gharama za Usafiri: Tsh 30,000/= zilitumika kufanikisha usafiri wa timu na uratibu wa huduma.
- Matumizi ya Kiutawala: Tsh 50,000/= zilitumika kutengeneza muhuri rasmi wa ofisi kwa ajili ya uratibu na utambulisho wa huduma hii.
Wajane waliopokea misaada hii wametoa shukrani zao za dhati kabisa kwa kila mmoja aliyeshiriki kufanikisha jambo hili kubwa la ufalme wa Mungu.
Asante sana kwa ushirikiano wenu mwema na sadaka zenu zinazoendelea kubadilisha maisha ya watu.
Mchungaji Isack Alphonce Gomugo
Huduma ya MAMM (mamm.co.tz)